Deuteronomy 28:4-9

4 aUtabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

5Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

6

bUtabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

7 c Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

8 d Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mwenyezi Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.

9 e Bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya Bwana Mwenyezi Mungu wako na kwenda katika njia zake.
Copyright information for SwhKC